Kocha Mkuu wa Geita, Hemmed Suleiman, amesema anautamani mchezo wao dhidi ya Yanga SC ili aweze kuendeleza rekodi ya ushindi aliyoanza nayo.
Amesema anawaheshimu Yanga lakini wao wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo kwenye mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kesho Oktoba 7, 2023.
"Kwanza tunamshukuru mwenyezi Mungu tuko salama, wachezaji wako vizuri tumefanya mazoezi yetu ya mwisho leo asubuhi na tuko tayari kucheza na Yanga, mechi itakuwa ngumu tunawaheshimu Yanga wana timu nzuri kwa takriban misimu mitatu iliyopita lakini na sisi tumeanza vizuri ligi tunataka kuendelea kufanya vizuri zaidi," alisema Hemmed.