Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita watacheza kwa morali ya juu

Yanga 3 Vs Geita 0 Geita watacheza kwa morali ya juu

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga vs Geita Gold FC ni mechi ambayo kila timu inapambania malengo yake, Yanga inapambania kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu lakini Geita Gold inapambana kutoka kwenye eneo la kucheza play off ili kibaki kwenye Ligi.

Kwenye makaratasi Yanga inapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huu lakini kwenye uhalisia huwezi kuinyima kabisa nafasi Geita Gold ya kupata walau alama moja.

Faida ambayo wanapata makocha wa timu za daraja la kati pindi wanapokutana na timu zinazoshindania ubingwa ni kwamba hawana kazi kubwa ya kuhamasisha wachezaji wao wanapokutana na timu aina ya Yanga, Simba au Azam.

Kwa hiyo unatarajia kuona wachezaji wa Geita Gold kuwa kwenye morali ya juu siku ya leo kwa sababu ili jina lako litajwe miongoni mwa wachezaji bora ni lazima uoneshe kiwango bora kwenye mechi kubwa.

Geita Gold inakutana na Yanga ambayo imeshinda mechi mbili zilizopita za Ligi Kuu ndani ya mwezi Machi, imeshinda dhidi ya Namungo na Ihefu, leo ni mchezo wa tatu kwa Yanga ndani ya mwezi huu kabla ya kuhitimisha dhidi ya Azam FC siku ya Jumapili.

Geita Gold ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi, ina alama 21 baada ya kucheza micjezo 20, imeshinda michezo mitano, sare sita na kupoyeza michezo tisa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: