Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita wanamuandalia mtu dozi

Fdrht Geita wanamuandalia mtu dozi

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha mkuu wa Geita Gold, Denis Kitambi amesema anatambua ugumu wa mchezo wake dhidi ya Simba Februari 12 huku akitamba kuwa kikosi chake kwa asilimia 60 kimeimarika na ana siku sita kumaliza 40 zilizobaki.

Kitambi ameliambia Mwanaspoti kuwa walikuwa na siku 14 za maandalizi mkoani Morogoro ambako wamepata nafasi ya kucheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar wakiibuka na ushindi wa bao 1-0.

Alisema kwa asilimia 60, kikosi chake kipo imara sasa anapambania 40 kabla ya kuivaa Simba ugenini katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

“Bado tuna muda wa kukiandaa kikosi, hii ni kutokana na mchezo wetu kuwa na siku sita nyingine mbele baada ya kufanya mazoezi kwa wiki mbili na kubaini asilimia 60 wachezaji wangu wapo imara;

“Uchezaji wa wachezaji wangu unaniridhisha, upungufu mdogo uliopo natakiwa kuufanyia kazi kabla ya kumvaa mnyama ambaye ni mzoefu kwenye ligi na anaweza kutumia makosa yetu kama mwanya wa kuibuka na ushindi.” alisema.

“Uwezo binafsi na kupambania nafasi kwa kila mchezaji ndio utakaonipa ugumu wa kuchagua nani aanze kikosini, kwa asilimia kubwa nina wachezaji wengi wazuri na wenye hali ya ushindani,” alisema.

Simba inacheza leo na Tabora United mechi ya kiporo,

Chanzo: Mwanaspoti