Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita uso kwa uso na Ihefu

Kikosi Geita Gold Cs Namungo.jpeg Geita uso kwa uso na Ihefu

Fri, 25 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Ligi kuu kusimama kwa siku ya jana Novemba 24, Leo Novemba 25 pia ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kwa mchezo mmoja ambapo Geita Gold ya Felix Minziro itakuwa ikikipiga dhidi ya Ihefu ya Mbeya.

Geita Gold ambayo ipo nafasi ya 7 huku wakiwa wameshinda michezo minne pekee, sare sita na kupoteza mechi tatu kwenye ligi hadi sasa na kujivunia pointi zao 18.

Wakati kwa Ihefu wao wakiwa bado na hali mbaya wapo nafasi ya mwisho kwenye Ligi wakiwa wamecheza michezo 12 lakini ushindi ni mara mbili pekee, wakienda sare mara mbili na kupoteza michezo nane na alama zao 8.

Mchezo huo wa leo unatarajiwa kupigwa katika uwanja wa Nyankumbu majira ya saa kumi jioni huku Ihefu akiuhitaji mchezo huo kwa hali na mali ili aweze kujinasua katika nafasi aliyopo.

Swali linakuja ni je ataweza kupata pointi tatu kwa Geita ambaye yupo kwenye kiwango kizuri akiwa kapoteza mechi chache zaidi yake huku ushindi wa leo akiuhitaji pia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live