Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita kifua mbele dakika 45 za kwanza

Half Pic Geita kifua mbele dakika 45 za kwanza

Mon, 13 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipindi cha kwanza kimemalizika katika Uwanja wa Nyankumbu Girls kwa wenyeji Geita Gold kuwa mbele kwa bao 1-0, dhidi ya Dodoma Jiji.

Kwenye mechi hiyo bao la Geita Gold, lilifungwa dakika ya tisa, na Edmund John baada ya kumalizia mpira uliotemwa na kipa wa Dodoma, Hussein Masalanga.

Bao hilo lilitokana na George Mpole kuchezewa rafu nje ya boksi na kupiga faulo aliyopiga kumlenga Masalanga na kushindwa kuokoa vizuri mpira huo na kwenda kumkuta mfungaji wa bao.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Geita walikuwa mbele kwao bao 1-0, na kuwafanya kutangulia kupata pointi tatu.

Kama mechi hiyo itamalizika hivyo Geita watafikisha pointi 39, na kupanda hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara hadi sasa.

Umuhimu wa kumaliza ligi kwenye nafasi ya tatu msimu huu kuna mkwanja wa maana kutoka Azam watapata pamoja na kupata nafasi ya kucheza mashindano ya kimataifa msimu ujao (Kombe la Shirikisho Afrika).

Kwenye mechi hiyo Geita walionekana kufanya mashambulizi mengi ya mara kwa mara kupitia kwa Mpole aliyeonekana kuwasumbua mabeki wa Dodoma.

Geita walikuwa bora kwenye ulinzi Juma Nyoso na Kelvin Yondani walikuwa nguzo muhimu ya kuzuia mashambulizi ya Dodoma Jiji.

Kwa upande wa Dodoma hawakufanya mashambulizi mengi ya mara kwa mara na kuonekana kupoteza mipira mingi na hawakuwa hatari kwenye mashambulizi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live