Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita bado haiamini, waitana fastaa

Geita Golddddddd Geita bado haiamini, waitana fastaa

Fri, 7 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kushuka daraja kutoka Ligi Kuu msimu huu na kuwa na ukimya kwa takribani wiki moja, uongozi wa Geita Gold umesema umeamua kutulia kwa sasa na kujikita kufanya vikao vya ndani ili kuja na maamuzi sahihi na mipango ya kinachofuata.

Timu hiyo ambayo ilidumu Ligi Kuu Bara kwa misimu mitatu tangu 2021/2022 hadi 2023/2024, imeshuka msimu huu baada ya kukamata nafasi ya 15 ikiwa na alama 25 katika mechi 30, ikishinda tano, sare 10 na kupoteza 15, huku ikifunga mabao 18 na kuruhusu 38.

Moja ya mambo yanayosubiriwa na mashabiki kutoka kwa uongozi wa Geita Gold baada ya timu kushuka ni kujua hatma ya benchi lao la ufundi, wachezaji na mipango ya kucheza Ligi ya Championship.

Akizungumzia kinachoendelea klabuni hapo, Afisa Habari wa Geita Gold, Samwel Dida alisema kwa sasa viongozi wanatafuta utulivu wa mawazo kwa kufanya kwanza vikao vya ndani vitakavyotoa uelekeo.

“Kwa sasa hakuna kipya kinachoendelea lakini tunaendelea na vikao vya ndani ambavyo havijawa na maamuzi. Tutakuja baadaye na taarifa iliyokamilika kuhusu nini tunakwenda kufanya kwahiyo mashabiki na wadau wetu wawe wavumilivu,” alisema Dida

Mmoja ya wachezaji wa timu hiyo (jina tunalo), alisema baada ya mechi ya mwisho na timu kushuka daraja wachezaji walitawanyika kila mmoja kurudi kwao, huku kukiwa hakuna taarifa ya nini kitafuata kutoka kwa uongozi.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Denis Kitambi akinukuliwa na Mwanaspoti hivi karibuni, alisema “kuhusu hatima yangu hilo ni suala ambalo baadaye tutakaa chini na bodi kuamua na mwisho wa siku mimi siamui, wanachoamua ni bodi wameridhishwa na kazi yangu au la.”

Chanzo: Mwanaspoti