Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita: Tuchangieni tusajili, hatuna pesa

Duh Geita Geita: Tuchangieni tusajili, hatuna pesa

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Wanawake ya Geita Queens inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara yenye Maskani yake Mkoani Geita imeshindwa kufanya usajili kwa Wachezaji kwa kukosa fedha pamoja na Mdhamini wa kuidhamini Klabu hiyo huku ikiomba Wadau kuwasaidia.

Akizungumza nasi ofisini kwake, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Geita (GEREFA), Salum Kurunge amesema hadi sasa zimesalia siku nane kukamilisha na kufungwa kwa dirisha la usajili lakini bado Timu hiyo haipo kambini kutokana na kukosa fedha pamoja na kukosa Mdhamini huku akiwaomba Wadau mbalimbali kujitokeza kuisaidia Timu hiyo.

"Tunawaomba Wadau wote kuichangia Timu yetu ili iweze kukamilisha usajili huku tukiendelea na mipango mingine kwa jili ya ushiriki wa Ligi kikamilifu, kulikuwa na ugumu wa kuichangia Timu Wadau wengi walikuwa na imani kuwa ipo chini ya Halmashauri na ina udhamini, niwaeleze Timu yetu haina Wadhamini na inahitaji sana Wadhamini.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live