Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita, Ihefu zamtaka Kibu Denis

Kibu Denis, Usajili Kibu Denis

Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Geita Gold imetuma ofa Simba ya kutaka saini ya mshambuliaji wake Kibu Denis kwa mkopo katika dirisha dogo la mwezi huu wa Desemba.

Imethibitika kuwa matajiri hao wa dhahabu wapo kwenye kusuka upya kikosi chao na pendekezo la kwanza kwenye eneo la ushambuliaji ni Kibu ambaye wanaamini atarithi mikoba ya George Mpole aliyetimkia FC Lupopo ya DR Congo.

Bado Simba na Kibu hawajajibu ombi hilo la Geita aliyoichezea kipindi ipo (Daraja la kwaza) kwa sasa Chamiponship kabla ya kujiunga na Mbeya City kisha Simba anayoitumikia kwa sasa.

Wakati huo huo taarifa kutoka Mbeya zinaeleza Ihefu nayo ipo kwenye hatua za mwisho za kutuma ofa Simba kumuomba Kibu kwa mkopo.

Kibu ndiye mfungaji bora wa msimu uliopita kwa Simba alipomaliza na mabao nane, na msimu huu hadi sasa ana bao moja alilolifunga juzi dhdi ya Geita wakati chama lake likiibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live