Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold yajitosa kwa Moloko

Moloko Jesus Ducapel Moloko

Tue, 16 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saa chache baada ya Yanga kutangaza kumtema winga Jesus Moloko Geita Gold iko naye mezani kwa mazungumzo ya kumsajili kwa mwaka mmoja.

Geita inamtaka Moloko kwenda kuongeza nguvu kwenye kikosi chao ikiutazama uzoefu wake na nidhamu kubwa aliyoonyesha akiwa Yanga.

Geita inapambana na Rayon Sport ya Rwanda kuwania saini ya winga huyo wa zamani wa AS Vita na Union Maniema zote za DR Congo.

Moloko ametemwa na Yanga kupisha usajili wa winga Mghana Augustine Okrah aliyetua klabuni hapo akitokea Bechem United ya nchini kwao.

Kwasasa Geita inapambana na Moloko juu ya mshahara wake na maslahi mengine binafsi wakati mazungumzo hayo yakiendelea.

Moloko bado anatamani kubaki zaidi Tanzania endapo atapata ofa nzuri itakayomshawishi kukubali mkataba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live