Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold yaitaka Yanga robo fainali

Geita Gold Waitaka Yangaaaa Geita Gold yaitaka Yanga robo fainali

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kufuzu robo fainali kwa kuinyoosha Rhino Rangers kwa mabao 2-1, benchi la ufundi la Geita Gold limesema lina hamu ya kupangwa na Yanga katika hatua hiyo ya michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC) ili kulipa kisasi dhidi ya watetezi hao wa taji.

Kocha Mkuu wa Geita, Denis Kitambi amesema matamanio makubwa waliyonayo ni kuona wanapangwa na Yanga katika robo fainali iwapo watetezi hao nao watapita mbele ya Dodoma Jiji.

Geita imefuzu hatua hiyo ikiwa ni timu ya pili baada ya Namungo kufanya hivyo mbele ya Kagera Sugar, kwa ushindi iliyopata katika mchezo wa 16 Bora wa michuano hiyo uliopigwa kwenye Uwanja wa Nyankumbu, mjini Geita shukrani kwa mabao ya Jonathan Ulaya na Elias Maguli, huku la Rhino likifungwa na Mack Samson.

Akizungumzia sababu ya kutamani kukutana na Yanga, Kitambi alisema lengo kubwa ni kutaka kusahihisha makosa, kwani katika misimu miwili mfululizo watetezi ndio wamekuwa kikwazo kwa timu hiyo kwenda nusu fainali.

"Tunaheshimu timu zote zilizopo kwa sababu ya ubora zilizokuwa nazo, tunahitaji kulipiza kisasi ndio maana kila mchezo huwa tunauchukulia kwa uzito mkubwa, malengo yetu sio kuishia tena hapa tulipofikia bali kusonga mbele zaidi," alisema Kitambi.

Msimu uliopita Geita ilitolewa na Yanga katika hatua ya robo fainali kwa kufungwa bao 1-0, lililopachikwa wavuni na aliyekuwa nyota wa kikosi hicho Mkongomani, Fiston Mayele katika dakika ya 57, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Aprili 8, 2023.

Msimu wa 2020/2021, Geita ilishindwa pia kutamba mbele ya Yanga katika hatua ya robo fainali kwa kuchapwa kwa mikwaju ya penalti 7-6 baada ya dakika 90 za mchezo huo uliopigwa Kwa Mkapa Aprili 10, 2022 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Geita ilifika hatua hiyo kwa kuiondosha Mbeya City katika hatua ya 32 bora na kuungana na Namungo katika robo fainali ya kombe hilo kufuatia kuiondosha Kagera Sugar kwa mikwaju ya penalti 5-3, baada ya kushindwa kutambiana ndani ya dakika 90.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: