Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold yaichapa Prisons

Geita Pic Data (600 X 469) Geita Gold watakata nyumbani

Thu, 23 Dec 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Klabu ya Geita Gold imetumia vyema uwanja wake wa Nyankumbu baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Maafande wa Tanzania Prisons.

Geita wamepata bao hilo baada ya kona safi iliyopigwa na Amosi Charles Kadikilo kisha nyota wa Prisons Adili Buha kujifunga dakika ya 51, wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa mpira.

Ushindi huo kwa Geita Gold unakuwa wa tatu msimu huu baada ya mchezo uliopita kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Ruvu Shooting na ule wa Kagera Sugar (2-1) Novemba 20.

Katika michezo iliyosalia walifungwa na KMC, (2-0), Simba (2-1), Azam FC (1-0), Yanga (1-0) na Namungo FC (2-0) huku ikitoka sare michezo miwili ya bao 1-1, dhidi ya Mbeya City, Mtibwa Sugar na kufikisha pointi 11, wakiwa nafasi ya tisa.

Kwa upande wa Tanzania Prisons unakuwa mchezo wa sita kati ya 10, waliyocheza kupoteza baada ya kufungwa na Yanga (2-1), Polisi Tanzania (1-0), Biashara United (3-0), Dodoma Jiji (2-1) na Mbeya City (1-0), wakishinda miwili tu ambao ni dhidi ya Namungo FC (3-1) na Mbeya Kwanza (2-1), huku michezo miwili wakitoka suluhu ya 0-0, kutoka kwa Coastal Union na Mtibwa Sugar.

Matokeo hayo kwa Maafande yanazidi kuwaweka sehemu mbaya kwenye msimamo kwani wamefikisha pointi nane wakiwa nafasi ya 15, baada ya kucheza michezo 10.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz