Klabu ya Geita Gold ikishirikiana na halmashauri ya Geita inaendelea na ujenzi wa uwanja wao wenye uwezo wa kubeba mashabiki 12,000. Kampuni ya Geita Gold imetoa Tsh 2.4bn za ujenzi kama awamu ya kwanza.
Huu ndio Uwanja wa Magogo wa Timu ya Geita Gold FC unajengwa chini ya Halmashauri ya Geita na Kampuni ya Geita Gold Mine ambao sasa Kwa awamu hii Utakuwa na:
1. Jukwaa Kuu VIP
2. Fence kubwa kuzunguka Uwanja
3. Fence ndogo kuzuia mashabiki kufika kwenye Pitch
4. Pitch ya Artificial Grass
5. Sehemu ya kukimbilia
6. Vyoo sehemu mashabiki watakuwepo kuzunguka
7. Vyumba vya Ofisi, Mikutano, Wachezaji, Wasimamizi wa michezo
8. Parking
NB: Gharama za awamu hii ni 2.4B na Watazamaji kwa sasa wa Mzunguko watakuwa Wanasimama, Malengo baadae kwa awamu zinazofuata ni kujenga majukwaa watu 12,000 kukaa.