Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold yachimba mkwara

Geita Gold Kitisho Kikosi cha Geita Gold kikiendelea na mazoezi

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Geita Gold imezipiga mkwara timu shiriki za Ligi Kuu Tanzania bara kwamba zisitegemee mteremko kwa mechi zake zitakazochezwa uwanja wake wa nyumbani wa Nyankumbu ulioko wilayani humo, ikiwemo Mtibwa Sugar utakaochezwa Jumamosi.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Geita Gold Fc, Hemed Kivuyo watacheza mechi hiyo kama nyati aliyejeruhiwa kwa sababu wamepoteza mechi mbili ambazo ni dhidi ya Namungo na Yanga.

Kivuyo amesema mchezo dhidi ya Mtibwa ni wa kwanza kuucheza kwenye uwanja wake wa nyumbani, wanapaswa kuutendea haki uwanja wake wa nyumbani.

Pamoja na kujigamba huko, mchezaji wao, Salum Ayee ni majeruhi ambaye hali yake inaendelea kuimarika.

Kivuyo alitumia fursa hiyo kumtangaza Shafii Omary 'JK comedian' kuwa balozi wa timu hiyo ambako pia wanatarajia kuwatangaza mabalozi wengine hivi karibuni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live