Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold yabeba alama tatu mbele ya Ruvu Shooting

Geita Gold Yashinda Geita yaichapa Ruvu Shooting

Fri, 17 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Geita Gold imeibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Primia Ligi) jioni ya leo katika Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.

Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Danny Lyanga dakika ya tatu na George Mpole dakika ya 90 na ushei, wakati la Ruvu Shooting alijifunga Nashon Naftali dakika ya 45.

Kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi nane na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya 14, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake tisa katika nafasi ya 11 baada ya timu zote kucheza mechi tisa sasa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live