Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold watinga Robo Fainali Azam Sports Federation

Geita Advance Kikosi cha Geita Gold

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Geita Gold imefanikiwa kutinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ikiungana na Simba iliyotangulia jana Alhamisi ikiichapa African Sports ya Tanga mabao 4-0.

Geita imetinga hatua hiyo leo Ijumaa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Green Warriors ya Dar es Salaam katika mchezo wa hatua ya 16 bora ambao umepigwa saa 10 jioni Uwanja wa Nyankumbu, Geita.

Wachimba Dhahabu hao wametinga hatua hiyo ikiwa ni mara ya pili mfululizo, ambapo msimu uliopita walifika hatua kama hiyo lakini wakaondolewa na Yanga ambayo ilitwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Katika mtanange wa leo, Geita Gold imepata mabao yake kupitia kwa kiungo, Jofrey Manyasi kwa mkwaju wa penalti dakika ya Saba, Dany Lyanga dakika ya 16 na Elias Maguri dakika ya 57.

Penalti aliyofunga leo kiungo Jofrey Manyasi ni ya pili mfululizo ambapo alifanya hivyo dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Ligi Kuu wakati timu yake ikishinda mabao 3-2 Uwanja wa Nyankumbu.

Bao ambalo amefunga Elias Maguli ni la tano kwake katika mechi saba alizocheza tangu ajiunge na Geita Gold dirisha dogo Januari, mwaka huu, ambapo amefunga mawili kwenye shirikisho na matatu Ligi Kuu.

Nahodha wa Geita Gold, Dany Lyanga amefunga bao tangu alivyofan6a hivyo Desemba 25, 2022 wakati timu hiyo ikipata sare ya 2-2 dhidi a Kagera Sugar katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Hilo ni bao lake la tatu msimu huu ambapo la kwanza alilifunga Septemba 17, 2022 kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya awali dhidi ya Al Hilal Sahil ya Sudan.

Bao ililoruhusu leo Geita Gold dhidi ya Green Warriors ni la kwanza kwenye michuano ya Shirikisho katika michezo mitatu waliyocheza ambapo waliichapa Transit Camp 1-0, Nzega United 1-0 na Green Warriors 3-1.

Kiungo wa Geita Gold, Shinobu Sakai raia wa Japan amecheza mchezo wake wa tatu msimu huu tangu alipotua kwenye timu hiyo dirisha kubwa huku ukiwa mchezo wake wa pili wa kombe la Shirikisho akicheza dhidi ya Nzega United, Green Warriors na Namungo FC.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live