Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold waanza tambo

Geita Gold Tambo Kokosi cha Geita Gold

Sat, 8 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Geita Gold tayari ipo jijini Dar es Salaam ikijifua kwa ajili ya mechi ya robo fainali ya Kombe la ASFC itakayopigwa leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, huku benchi la ufundi na mastaa wa timu hiyo wakiweka bayana kwamba wapo tayari kumalizana na wenyeji wao kibabe.

Yanga na Geita zinakutana ikiwa ni wiki kadhaa tangu zilipovaana kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara na vijana wa Jangwani waliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Pamoja na ugumu wa pambano hilo, kocha wa Geita, Fred Felix ‘Minziro’ amesema amewapa mbinu zote wachezaji wake kwani anajua wanakutana na vigogo, lakini wamejipanga kupambana kiume ili kupata ushindi kwa mara ya kwanza mbele ya Yanga, aliyokiri ina kikosi imara.

“Huwa nawaambia wachezaji kutorudia makosa ambayo wameyafanya katika michezo iliyopita hii ndio njia pekee wanaweza kushinda kama watarekebisha makosa.

Matumaini yetu ni kufanya vizuri kwani hatuishi na matokeo ya yaliyopita kwani mchezo huu kwao ni mpya kabisa,” alisema kocha aliyewahi kuwa nyota na kocha wa Yanga sambamba na kuzinoa timu nyingine kadhaa nchini.

Kwa upande wa beki, George Wawa amesema; “Kambini tukikaa tunapeana mikakati ya kupambana kwa nguvu na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri. Huu sio mchezo rahisi ukizingatia walitufunga mara ya mwisho tulivyokutana nao.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live