Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold kamili kuivaa Polisi

Yondani Geita G Geita Gold kamili kuivaa Polisi

Thu, 19 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benchi la ufundi la Klabu ya Geita Gold limesema limejipanga vizuri kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya timu ya Polisi utakaopigwa kesho Ijumaa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Fred Minziro alisema wachezaji wote wanaendelea vizuri kuelekea kwenye mchezo huo ambao amekiri kuwa utakuwa na upinzani mkubwa.

“Tumejiandaa kukutana na timu ya Polisi na tumeupa umuhimu mkubwa mchezo huo licha ya kwamba wapinzani wetu wapo nafasi za chini katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara,” alisema Minziro.

Kocha huyo alisema usajili walioufanya msimu huu utaleta ushindani ndani ya kikosi chake hicho na kudai malengo yake ni kushika nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema anaridhishwa na viwango vinavyoonyeshwa na wachezaji wake nje na ndani ya uwanja jambo ambalo linampa matumaini ya kuendelea kuinoa timu yake hiyo na kuwataka mashabiki wake waendelee kuwapa ushirikiano.

Alisema ligi msimu huu ina ushindani mkubwa kila timu imejipanga kupata matokeo mazuri hivyo atapambana kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michezo yao iliyobakia msimu huu ili atimize malengo yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live