Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold imeanza kujipata

Geita Gold FC CEO.jpeg Geita Gold imeanza kujipata

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Geita Gold, Denis Kitambi ameonyesha kufurahishwa na namna timu hiyo inavyocheza sasa tofauti na kipindi cha nyuma.

Kitambi ambaye ajiunga na Wachimba Dhahabu hao akichukua nafasi ya Hemed Suleiman 'Morocco' aliyefungashiwa virango ameiongoza timu hiyo katika mechi tatu akishinda moja na kuchezea vipigo viwili.

Mechi hizo ni dhidi ya Singida Fountain Gate (1-0), Simba (0-1) na Azam FC (2-1) inayoifanya timu hiyo kushika nafasi 13 kwa alama 16 baada ya mechi 15,,imeshinda nne sawa na mechi ambayo imetoka sare huku ikipoteza saba.

Kitambi alisema baada ya kazi kubwa ambayo amefanya ikiwemo kuwaongeza nyota kadhaa kwenye kikosi kwa sasa timu inabadiliko makubwa hasa ya kiuchezaji.

Alisema kadri siku zinavyosogea anaamini kila kitu kitakuwa sawa na Geita itarudisha ule ubora wake ambao wengi wameuzoea na kuweza kumaliza nafasi za juu ambayo ndio malengo yao.

“Katika mechi zilizopita timu ilikuwa inatetereka sana lakini sasa hali hiyo hakuna hivyo utaona ni kwa namna gani mabadiliko makubwa yamefanyika,” alisema Kitambi.

Aliongeza, hata umiliki wa mpira na namna timu inavyocheza sasa inampatia matumaini makubwa sana kama mwalimu hasa katika kupambania malengo wakati huu ambapo timu zote 16 zimeanza kucheza mechi zao za mzunguko wa pili.

Kitambi aliweka wazi kuwa kitu kingine ambacho kama mwalimu atafanyia kazi ni kukabiliana na mipira ya krosi ambayo kwenye mchezo wa Azam iliwanyima kupata matokeo baada ya timu yake kupoteza.

Chanzo: Mwanaspoti