Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold ikishindwa kupanda kuna mkono wa mtu

Geita+pic.png Geita Gold ikishindwa kupanda kuna mkono wa mtu

Thu, 8 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By YOHANA CHALLE MAMBO yameanza kuiva huko Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayotarajia kutimua vumbi wikiendi hii katika msako wa timu mbili zitakazopanda moja kwa moja Ligi Kuu msimu ujao.

Kwa taarifa yako wachimba madini kutoka Geita, Geita Gold wametamba tayari wanachukua nafasi moja hivyo wapinzani wake watangoja hatua ya mtoano. Geita Gold ni moja ya timu tishio FDL na inapokutana na wapinzani wao hupaswa kujipanga vilivyo.

Msimu huu mambo yamekuwa tofauti kuanzia benchi la ufundi ili kuhakikisha kikosi hicho kinakuwa tishio zaidi. Baada ya Gipco FC kupigwa bei sasa inawafanya wachimba madini hao kubaki wenyewe na kukusanya mashabiki wa mkoa wote kuwasapoti kwenye mbio za kuwania safari ya kuelekea Ligi Kuu.

WAMEJIPANGA

Ofisa Habari wa timu hiyo, Gabril Gabo anasema usajili walioufanya na mabadiliko ya benchi la ufundi vinawapa jeuri kupambana na kujipa matumaini ya kupanda Ligi Kuu. “Misimu miwili tumeishia hatua ya mtoano na tumeonyesha kiwango kikubwa kwa muda wote huo, hivyo tunaamini msimu huu kila kitu kitakwenda sawa,” anasema.

“Timu ilianza mazoezi mapema chini ya Kocha Fred Minziro, na asilimia kubwa ya wachezaji wapo fiti, kikubwa ni mapambano pekee yanayongojewa kwa sasa.”

Chanzo: mwanaspoti.co.tz