Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold: Yanga mjipange haswa

Yanga Mjinange Yanga wanajiandaa kukutana na Geita Gold FC, Robo Fainali Azam Sports Federation

Sat, 9 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Geita Gold, Fred Felix ‘Minziro’ amesema mchezo wao ujao wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) hatua ya robo fainali dhidi ya wapinzani wao Yanga wasitarajie mteremko.

Timu hizo zitakutana Jumapili hii ya Aprili 10, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku Minziro akiweka wazi malengo yao ni kucheza fainali kwa mara ya kwanza.

“Tunawaheshimu Yanga ni timu nzuri na imeshatufunga mara mbili msimu huu ila hii ni mechi nyingine na maandalizi ni ya tofauti kabisa kwa sababu ni hatua ya mtoano na tumejipanga kulipiza kisasi,” alisema Minziro ambaye ni staa na kocha wa zamani wa Yanga.

“Mashindano haya yanakupa nafasi ya uwakilishi wa nchi kimataifa hivyo ni lazima kucheza kwa mikakati imara ya kuzuia na kushambulia kwa tahadhari huku tukiziba mianya yote itayowapa nafasi ya kutengeneza nafasi za kutushambulia,” aliongeza.

Katika michezo yote miwili ya Ligi Kuu ambapo timu hizo zilikutana, Yanga ilishinda bao 1-0 kwa mechi zote na sasa zitakutana Jumapili na mshindi ataungana na mshindi wa mechi ya Aprili 13 kati ya Simba na Pamba kucheza nusu fainali.

Geita ilifika robo fainali ya ASFC kwa kuifunga Mbuni kwa bao 1-0, katika hatua ya 16, bora wakati Yanga ikiichapa Biashara United mabao 2-1 jijini Dar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live