Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold: Tutaiogopaje Yanga timu ambayo haina hata Uwanja?

Hemed Kivuyo Geita Afisa Habari wa Geita Gold, Hemed Kivuyo

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Geita Gold ikiwa imetoka kupokea kichapo cha magoli 3-1 mchezo wa Ligi Kuu Bara Uwanja wa Azam Complex.

Hatimaye Geita Gold wamepata nafasi ya kulipa kisasi baada ya kupangwa tena na Yanga katika mchezo wa Robo Fainali ya Michuano ya Azam Sports Federation.

Sasa akizungumza Afisa Habari wa Geita Gold, Hemed Kivuyo amesema;

“Hatuiogopi Yanga, Ni timu kongwe tu lakini kwa ubora hawajatuzidi, Tutaiogopaje Timu tunayoizidi kiuchumi? Tutaiogopaje Timu haina hata uwanja wao. Tupo tayari kupambana nao Robo Fainali na kufuzu kwenda Nusu Fainali”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live