Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold, Namungo zasonga mbele ASFC

IMG 7957.jpeg Geita Gold, Namungo zasonga mbele ASFC

Sun, 17 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Geita Gold imefanikiwa kutinga Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Singida Cluster katika mchezo uliofanyika leo Uwanja wa shule ya sekondari ya wasichana ya Nyankumbu mjini Geita.

Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Tariq Seif dakika ya 14 na 19, Mwaita Gereza dakika ya 47, George Sangija dakika ya 49 na Geofrey Julius dakika ya 90 na ushei.

Mechi nyingine za ASFC leo, Namungo imeitupa nje Hollywood kwa kuichapa mabao 5-0 Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.

Mabao ya Namungo FC yamefungwa na James Mwashinga dakika ya 23, Kelvin Sabato dakika ya nane kwa penalti, 36 na 63 na Michael Joseph dakika ya 77.

Nayo Tabora United imeichapa Coffee ya Mwadui 4-1 Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora huku jirani zao, Mashujaa FC wakiilaza Mbuga FC 3-2 Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

MATOKEO YOTE MECHI 64 BORA ASFC

DESEMBA 16, 2023

Namungo FC 5-0 Hollywood FC

Geita Gold 5-0 Singida Cluster

Mashujaa FC 3-2 Mbuga FC

Tabora United 4-1 Coffee Monduli

Pan Africans 1-2 Nyamongo SC

Biashara United 4-1 THB FC

FGA Talents 2-0 Buhaya FC

Polisi Tanzania 2-1 Nyumbu FC

Pamba FC 1-0 Eagles SC

Green Warriors 4-1 Kilimo FC

Mbuni FC 6-2 Bus Stand

Tanzania Prisons 0-0 TRA Kilimanjaro (Penalti 5-6) DESEMBA 15, 2023 Singida Fountain 3-0 Arusha City

Ken Gold 0-1 Gunners FC

Transit Camp 2-0 Airport FC

Cosmopolitan 1-2 Rhino Rangers imewatoa

DESEMBA 14, 2023

Dodoma Jiji FC 1-0 Magereza Dar

JKT Tanzania 5-0 Kurugenzi Simiyu

Ihefu SC 3-0 Rospa FC

Coastal UniĆ³n 2-0 Greenland

MECHI ZA LEO DESEMBA 17, 2023

Mbeya City v African Lyon Sokoine, Mbeya

Cocpo FC v Mabao FC Nyamagana, Mwanza

Ruvu Shooting v Mkwajuni FC Jamhuri, Morogoro

TMA FC v Sharp Lion, Sheikh Amri Abeid, Arusha

KMC FC v ACA Eagle Uhuru, Dar es Salaam

Azam FC v Allianve FC, Azam Complex, Chamazi

MECHI ZA MWISHO ZITATAPANGIWA TAREHE

Yanga SC v Housing FC (Njombe)

Simba SC v Tembo FC (Tabora)

Mtibwa Sugar v Nyakagwe (Geita)

Kagera Sugar v Dar City

Chanzo: www.tanzaniaweb.live