Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold, Kitayosce wapambana kuinasa saini ya Mpole

Tdrt Mpole George Mpole

Fri, 30 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara, Msimu wa 2021/2022, George Mpole msimu ujao huenda akaendelea alipoishia baada ya Ligi Kuu DR Congo alikokuwa akicheza kwenye kikosi cha FC Lupopo kusimama kwa sababa za kiuchumi na vita na sasa yupo Bongo huku Geita Gold na Tabora United zikimpa ofa ya kutua katika vikosi vyao.

Mpole alikuwa mfungaji bora msimu wa 2021/2022 baada ya kumaliza na mabao 17 akiichezea Geita Gold mbele ya Fiston Mayele wa Yanga aliyekuwa na mabao 16, na baada ya hapo alitimkia Lupopo ya DR Congo kabla ya sababu za kiuchumi kuifanya ligi hiyo kusimama na Mpole kurudi Bongo.

Licha ya kwamba bado ana mkataba na Lupopo, lakini tayari timu yake ya zamani Geita Gold na Tabora United zamani Kitayosce iliyopanda Ligi Kuu msimu huu zimeonyesha nia ya kutaka kumpa mkataba baada ya kugundua ana ruhusa maalumu ya kucheza.

"Tunatafuta Mshambuliaji, yupo Mpole kwa sasa na tumejaribu kuongea naye licha ya kwamba hatujafika mwafaka kwani anatakiwa pia na timu yake ya zamani (Geita), tunazidi kusukuma usajili huu ufanikiwe licha ya kwamba utakuwa wa muda na kama Ligi itarejea DR Congo itabidi arudi Lupopo," alisema moja ya viongozi wa Kitayosce (jina tunalo).

Kwa upande wa Mpole alisema kwa sasa bado hajaamua atacheza wapi msimu ujao.

"Nikipata timu naweza kucheza ili kuendelea kutunza kiwango changu lakini kwa sasa siwezi kusema naenda wapi licha ya kwamba kuna ofa ninazo," alisema Mpole.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live