Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold, KMC hakuna mbabe, Saido gari limewaka

Saido Ntibazonkiza 1 Mchezo wa Geita Gold vs KMC umemalizika kwa sare ya magoli 1-1

Fri, 11 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezo kati ya Geita Gold na KMC umemalizika kwa kutoshana nguvu ya sare ya magoli 1-1 huku magoli hayo yakifungwa na Ntibazonkiza kwa wachimba dhahabu huku vijana wa Kino boys likifungwa na Waziri 'Junior' Shentembo

Nahodha na Mshambuliaji wa kikosi cha Geita Gold, Ayoub Lyanga ameukosa mchezo wa leo dhidi ya KMC baada ya kupata kadi tatu za njano.

Kikosi cha Geita Gold leo kilishuka dimbani kumenyana na KMC ukiwa ni mchezo wa ligi kuu kwenye Uwanja wa Nyankumbu, Geita.

Lyanga alipata kadi za njano kwenye mechi tatu dhidi ya Yanga, Polisi Tanzania na Coastal Union.

Geita Gold inayonolewa na Kocha Mkuu, Fred Minziro imekusanya pointi 14 pekee baada ya kucheza mechi 11.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live