Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold: Haturudii makosa

Geita Gold FC Caf.jpeg Kikosi cha Geita Gold

Fri, 16 Sep 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kocha Msaidizi wa Geita Gold, Mathius Wandiba amesema hawatarajii kurudia makosa waliyoyafanya mechi iliyopita wanahitaji ushindi ili waweze kusonga hatua inayofuata.

Geita Gold wanatarajia kuwa wenyeji wa Hilal Alhasil ya Sudan kesho mchezo unaotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 ugenini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Wandiba alisema wamefanyia kazi makosa waliyoyafanya mechi iliyopita wanatarajia mchezo mzuri na wa ushindani kutokana na ubora wa wapinzani wao.

“Wapinzani wetu ni wazuri na sisi ni bora pia tunatarajia ushindani mkubwa lani malengo yetu kama klabu ni kupata matokeo kwenye uwanja wetu wa nyumbani,” alisema.

Akizungumzia suala la kinara wa mabao, George Mpole ambaye alikosekana mechi iliyopita alisema anaendelea vizuri na amefanya mazoezi ya mwisho na timu suala la kucheza au kuto kucheza wao kama benchi la ufundi wataamua.

“Geita Gold kukosa matokeo kwenye mechi ya kwanza haina uhusiano wowote na kukosekana kwa Mpole kwani timu ina kikosi kipana lakini kurejea kwake itategemea na namna tutakavyopanga kikosi anaweza akachesa au asicheze.”

Alisema wachezaji wao wote wapo kwenye hali nzuri ya mchezo hawatarajii kumkosa mchezaji yoyote kutokana na ugonjwa au majeruhi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz