Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geita Gold, Azam FC hakuna mbabe

Geita Vs Azam 1 1.jpeg huu ni mchezo wa pili mfululizo Azam analazimishwa sare

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Geita Gold wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.

Ni wageni, Azam FC waliotangulia kwa bao la mshambuliaji wake Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 15, kabla ya kiungo Offen Francis Chikola kuisawazishia Geita Gold kwa penalti dakika ya 69.

Kwa matokeo hayo, Geita Gold inafikisha pointi 23 na kusogea nafasi ya sita, wakati Azam FC sasa ina pointi 37, baada ya wote kucheza mechi 17, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa mabao na Simba SC ambayo ina mechi moja mkononi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live