Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geay akamilisha safari Olimpiki, kuondoka leo

Olimpic Pic Data Mume Amuua Mkewe Kisha Kujinyonga

Fri, 14 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Hatimaye mwanariadha wa timu ya taifa, Gabriel Geay amekamilisha mchakato wa safari ya Italia kwa ajili ya kutafuta viwango vya Olimpiki.

Mwanariadha huyo ambaye awali alikuwa mguu ndani mguu nje kwenda nchini humo amefanikiwa kupata visa jana jioni ya leo Mei 13 ataondoka nchini na ndege ya Shirika la Ethiopia tayari kwa mbio za Generali Milano Marathon za Jumapili.

Geay mwanariadha nyota wa timu ya taifa kwenye mbio ndefu za uwanjani msimu huu atachuana kwenye marathoni kusaka viwango vya Olimpiki.

Hadi jana Jumatano Asubuhi mfukuza upepo huyo hakuwa na uhakika wa safari hiyo kutokana na mchakato wa kupata visa kuchelewa.

"Nimefanikiwa kupata jioni hii 'jana saa 12' hivyo niko safari kutoka Dar es Salaam kurejea Arusha ili kujiandaa na safari kesho (leo)," alisema mwanariadha huyo jana usiku akielezea mchakato wa safari yake.

Akizungumzia maandalizi ya safari hiyo, Geay alisema ataondoka leo saa 11 jioni kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA).

"Nitawasili Italia kesho (Ijumaa) na kupata muda kidogo wa kupumzika na kufanya maandalizi madogo madogo Jumamosi na Jumapili nitachuana kutafuta tiketi ya Olimpiki kwenye mbio za Generali Milano Marathon," amesema.

Geay ni miongoni mwa wanariadha 20 walioitwa kwenye timu ya taifa inayojiandaa na Olimpiki, ambao kati yao ni Alphonce Simbu na Failuna Abdi ndiyo wamefuzu kushiriki Olimpiki na wengine 18 wakitakiwa kutafuta viwango vya michezo hiyo akiwamo Natalia Elisante ambaye pia atachuana Jumapili nchini Italia.

Makamu wa rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), John Bayo amesema mbali na Geay na Natalia, Jackline Sakilu na Michael Kishiba pia wamepata mbio za marathoni nchini Afrika Kusini.

Bayo amesema bado wana changamoto ya kupata mbio za uwanjani (mita 100 hadi 10,000) kwa ajili ya wanariadha wao kutafuta viwango vya Olimpiki msimu huu kutokana na changamoto ya corona.

"Tuliomba Marekani, tumekosa, changamoto ya covid imevuruga vitu vingi, hivyo tunajaribu kuona kama Afrika Kusini watakuwa na mbio inayotambulika kidunia ili wanariadha wetu wa track 'mbio za uwanjani' wakatafute viwango huko,".

Aliwataja wanariadha wa mbio za uwanjani ambao wameitwa kwenye timu ya taifa kuwa ni Josephat Panga, Faraja Damas na Angelina Tsere.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz