Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gaya atemwa dakika za lala salama kikosi cha Hispania

Gaya Out World Cup.jpeg Jose Gaya

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Uhispania ikiwa tayari nchini Qatar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia itakayoanza rasmi Novemba 20, 2022 imethibitisha kuwa mchezaji wake Jose Gaya ameondolewa kwenye kikosi hicho baada ya kupata jeraha la mguu.

Beki huyo wa kushoto wa Valencia aliumia kifundo cha mguu Jumatano usiku akiwa mazoezini, lakini taarifa za awali ni kwamba jeraha hilo halikuwa kubwa.

Jana meneja wa Spain, Luis Enrique alithibitisha kuwa watachukua uamuzi kuhusu utimamu wa Gaya watakapowasili Qatar.

Lakini leo Spain wametangaza kuwa Gaya ataondoka kambini kutoka na jeraha hilo la mguu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live