Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gaucho awafuata Phiri, Mbombo

Abdulhalim Humud Abdulhalim Humud 'Gaucho'.

Thu, 22 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Mtanzania Abdulhalim Humud 'Gaucho' amejiunga na klabu ya Konkola Blades ya Ligi Kuu Zambia na kuwa mchezaji wa tatu kutoka nchini kutua kwenye ligi hiyo katika kipindi hiki baada ya Moses Phiri aliyekuwa Simba kujiunga na Power Dynamos na Idriss Mbombo aliyekua Azam kutua Nkana Red Devils.

Phiri ametua Dynamos kwa mkopo akitokea Simba akiwa ametoka kufunga mabao matatu kwenye Ligi Kuu Bara kwa msimu huu, huku Mbombo ameachana na Azam akitoka kuifungia mabao manane msimu uliopita baada ya kuanza msimu huu akiwa majeruhi na kukosa namba mbele ya nyota wapya waliosajili na kukimbilia Nkana.

Kwa upande wa Humud ameanza kazi kwenye timu yake hiyo inayoshika nafasi ya 11, kwenye ligi ya Zambia yenye jumla ya timu 18, ikiwa na alama 26 ilizovuna katika mechi 11 baada ya kushinda tano, sare 11 na kupoteza tano.

Homud amejiunga na timu hiyo kama mchezaji huru lakini kabla ya hapo aliwahi kuzichezea timu mbalimbali ikiwemo Simba, Azam, Ashanti United, Mtibwa Sugar, Sofapaka (Kenya), Coastal Union, Real Kings (Afrika Kusini), Majimaji FC, Namungo na Fountain Gate FC, sambamba na timu ya taifa, 'Taifa Stars'.

Kabla ya kutua Zambia, Humud alikuwa na zaidi ya miezi sita bila kucheza mechi za mashindano baada ya kuachana na Fountain Gate na wakati wote huo alikuwa akijifua kwenye viunga vya Azam Complex na baadhi ya timu zilizotumia uwanja huo kwa mazoezi.

Humud huenda akaanza kuitumikia timu hiyo mpya kwenye mechi za mashindano katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zambia, Jumamosi, Februari 24 na chama lake litakuwa ugenini kuvaana dhidi ya Green Buffaloes.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live