Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gatusso Kocha mpya Valencia

Gennaro Gattuso Gennaro Gattuso

Fri, 10 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa AC Milan na Italia, Gennaro Gattuso, 44 rasmi ametangazwa kama kocha mpya wa Valencia licha ya awali mashabiki kupinga maamuzi hayo.

Mtaliano huyo ambaye amevifundisha vilabu vya Napoli na AC Milan inakuwa ni mara yake ya kwanza kufundisha nje ya nchi yake na amesaini mkataba wa miaka miwili mpaka mwaka 2024.

Kiungo huyo wa zamani wa Italia anajiunga na Valencia kuchukua nafasi ya Jose Bordalas ambaye aliachana na klabu hiyo mapema mwezi huu baada ya msimu kukamilika.

Gattuso hakuwa na timu tangu Mei 2021 alipoondoka Napoli baada ya kuiongoza kushinda taji la Coppa Italia. Mwaka 2021 alitajwa kupewa nafasi ya kuifundisha klabu ya Fiorentina lakini mkataba ulivunjwa kabla ya kuanza kuinoa timu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live