Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gattuso atupiwa virago Olympique Marseille

Gattusso Afukuzwa Gennaro Gattuso

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Olympique Marseille imemfuta kazi mkufunzi Gennaro Ivan Gattuso Ufficiale kama kocha mkuu klabuni hapo kufuatia mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo ikiwemo kipigo cha 1-0 dhidi ya Brest kwenye Ligi Kuu Ufaransa siku ya Jumapili Februari 18, 2024.

Gattuso amedumu katika Klabu ya Olympique Marseille kwa siku 144 (tangu Septemba 27, 2023 hadi Faberuari 19, 2024) ikiwa ni timu ya pili kutimuliwa baada ya kufanywa hivyo Januari 30, 2023 na Valencia.

Kocha Jean-Louis Gasset (70) raia wa Ufaransa ambaye alifutwa kazi kama kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast wakati wa michuano ya AFCON 2023 anapigiwa upatu kuchukua mikoba ya Gattuso.

Jean-Louis Gasset alifutwa kazi kama kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ivory Coast kufuatia mwanzo mbaya kwenye michuano ya kombe la Mataifa Afrika kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Emerse Faé aliyewaongoza ‘The Elephants’ kutwaa AFCON 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live