Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gary Neville akosoa Manchester United inavyoshughulikia uchunguzi

Gary Neville Akosoa Manchester United Inavyoshughulikia Uchunguzi Gary Neville akosoa Manchester United inavyoshughulikia uchunguzi

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: Bbc

Gary Neville anasema jinsi Manchester United inavyoshughulikia uchunguzi wa Mason Greenwood imekuwa hatua ya "ya kutisha sana" na haina uongozi thabiti.

Greenwood, 21, ataondoka katika klabu hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili baada ya uchunguzi wa ndani wa miezi sita.

Ilikuja baada ya mashtaka dhidi ya mchezaji huyo, ikiwa ni pamoja na kujaribu kubaka na kushambulia,kuondolewa mwezi Februari.

"Ilikuwa wazi tangu siku ya kwanza kwamba hataichezea Manchester United tena," alisema beki wa zamani Neville.

Akizungumza kwenye Sky Sports Monday Night Football, Neville, 48, ambaye alichezea mechi 602 , aliongeza:

"Mchakato wa kufika huko umekuwa mbaya sana. Unapokuwa na hali muhimu, na hali ngumu kama hii, inahitaji uongozi thabiti wenye mamlaka. Na hiyo inatoka juu sana. Manchester United hawana hilo."

Mchambuzi mwenzake na kiungo wa kati wa zamani wa England Karen Carney alisema suala hilo "lilishughulikiwa vibaya" na ilikuwa "hali isiyofurahisha sana kwangu".

Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Greenwood alikamatwa Januari 2022 kufuatia madai kuhusu nyenzo ambayo ilichapishwa mtandaoni.

Chanzo: Bbc