Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gary Neville: Presha imeanza kumdhuru Raya

Image 330.png Gary Neville: Presha imeanza kumdhuru Raya

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Gwiji wa Soka nchini England Gary Neville anaamini PRESHA inaanza kumpata Mlinda Lango chaguo la kwanza katika kikosi cha Arsenal, David Raya na anazidi kufanya makosa.

Raya alikuwa na wakati mgumu katika mechi ya Arsenal kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Lens na kujiamini kwake kulipata pigo jingine alipofungwa na Mykhailo Mudryk katika sare ya mabao 2-2 ya Arsenal dhidi ya Chelsea kwenye Ligi Kuu England, mwishoni mwa juma liulilopita ( Jumamosi – Oktoba 21).

Neville, ambaye alikuwa mchambuzi katika mechi hiyo ya dabi ya London, anahisi kwamba kiwango cha Raya tangu kumpokonya nafasi aliyekuwa Mlinda Lango chaguo la kwanza klabuni hapo Aaron Ramsdale kinaanza kumpa presha raia huyo wa Hispania.

“David Raya alianza soka lake pale Arsenal vema, lakini baadae akawa na mchezo mbaya wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (dhidi ya Lens) ikifuatiwa na kipindi cha kwanza dhidi ya Manchester City,” amesema Neville wakati akizungumza na Sky Sports.

“Sasa presha inazidi kuwa kubwa kwake,” amesema.

“Ni nafasi ngumu zaidi kucheza na hakika unapokuwa katika moja ya klabu kubwa kwenye ligi, unaangaliwa zaidi hasa kama wewe ni Mlinda Lango.

“Mikel Arteta ameunda hilo, tuwe wazi na hali ya Ramsdale na Raya. Si kawaida, lakini inaweza kufanya kazi.

“Sijawahi kuamini inaweza, na ninaamini tunaona mbele ya macho yetu changamoto zilizopo kwa sababu sasa, kutakuwa na shinikizo.

“Aaron Ramsdale hakuwa amefanya makosa mengi mwanzoni mwa msimu. Raya sasa ameanza kufanya makosa.”

Ramsdale hajaficha kufadhaika kwake kwa kushindwa kuichezea Arsenal, si haba kwa sababu anahofia nafasi yake katika kikosi cha England kwa ajili ya michuano ya Ulaya msimu ujao.

Chanzo: Dar24