Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gary Neville: Pale Man United kuna tatizo kubwa

Gary Neville Gary Neville: Pale Man United kuna tatizo kubwa

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji nguli wa soka na mchambuzi wa masuala ya soka barani Ulaya, Gary Neville amesema kuwa kuna tatizo ndani ya Klabu ya Manchester United ambayo imekuwa ikifanya vibaya kwa takribani miaka 10 sasa.

"Erik ten Hag ni meneja mzuri sana, tunajua hilo, hatuwezi kupinga hilo. José Mourinho ni meneja mzuri, hatuwezi kupinga hilo. Tunachopaswa kujiuliza ni sababu ya kuendelea kushindwa katika klabu hii.

"Sio kwa sababu ya mchezaji mmoja au uwezo wake. Ni kushindwa kwa kitamaduni, na ndivyo hivyo. Tumeona mameneja wakubwa na wachezaji wa soka wakija kwenye klabu hii na kufa mbele ya macho yetu.

"Kwa kweli ninaamini kuna sumu kwenye klabu hii, inakula kila meneja anayekuja na kila mchezaji anayekuja.

"Harry Maguire alitakiwa kwenda Manchester City, Mason Mount alitakiwa kwenda Liverpool. Watazame sasa, wako makaburini," Gary Neville.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live