Kumekucha. Alejandro Garnacho amebonyeza kifute cha ‘like’ kwenye posti inayomshambulia kocha wa Manchester United, Erik ten Hag kwa kitendo chake cha kumtoa wakati wa mapumziko katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu England dhidi ya Bournemouth.
Kocha huyo wa Man United, Mdachi Ten Hag anashutumiwa kuwaogopa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi kwenye klabu hiyo na badala yake amekuwa akiwaondoa makinda kama Garnacho na kuwatoa katika mechi hiyo ya sare ya 2-2.
Kilichowashtua wengi ni kitendo cha kinda huyo wa Kiargentina, Garnacho, 19, kuguswa na kuonekana kupendezwa na posti hiyo inayomponda kocha wake ambayo ilipostiwa na Mark Goldbridge, shabiki maarufu wa Man United anayejihusisha zaidi na mtandao wa YouTube.
Shabiki mmoja aliandika kwenye mtandao wa X: “Lol Garnacho amelike hii. Kitanuka Man United.” Goldbridge aliposti: “Ten Hag amemshushia lawama Garnacho kwenye mkutano wa waandishi baada ya mechi.
Sio vizuri kumwonea dogo wa miaka 19 kwa ubora wote anaoonyesha msimu huu. Lakini, kubwa ameonyesha tena kuogopa kuwavuruga wanaolipwa mishahara mikubwa (Rashford).