Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Garnacho; Nuru inayoishi na dhambi

Garnacho Decide Argentina Alejandro Garnacho

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Achana na Dhambi ya Asamoah Gyan kushindwa kuipeleka Timu ya Taifa ya Ghana Nusu fainali pale kwa Madiba aaah wanangu hiyo sio Dhambi kubwa kuliko hii.

Kuna muda unajisemea mwenyewe hivi kuna Dhambi kubwa kama ile ya Luis Figo kuihama Barca na kuhamia kwa watani wao Real Madrid hadi ikapelekea Figo kutupiwa kichwa cha nguruwe kipindi anapiga kona, aah hiyo ya Figo sio Dhambi.

Vipi Dhambi ya Mauro Icard kumuibia mke mshikaji wake Max Lopez, hiyo sio Dhambi kubwa sana kama Dhambi hiii.

Yees ni dhambi kubwa ya Alejandro Garnacho kusema yeye anamkubali Cristiano Ronaldo kama Idol wake kuliko Muargentina mwenzake Lionel Messi, pale Argentina Garnacho ni nuru iliyo na Dhambi kama ya Yuda kumsaliti Yesu.

Garnacho anasemwa sana kule Argentina na kila mtu kuanzia Magwiji wa timu hadi mashabiki, kuna siku dogo alipost akisema Ronaldo ndiye GREATEST OF ALL TIME duuuh Aguero alimjia juu sana Garnacho.

Waargentina walilia sana na tukio hili la Alejandro maana ilifikia hatua mashabiki wa Ronaldo wakaja na sera yakuwa kama raia wenzake wa Argentina hawamjui Messi kama G.O.A.T vipi sisi tumuite G.O.A.T, Garnacho ni nuru ya kipaji cha mbeleni pale Argentina lakini wenyewe ambao wanamuita Ki home Boy wanamuona ana dhambi kubwa.

Lakini Argentina wanamkosea Garnacho, sasaivi tupo kwenye kizazi cha Matozi + Kipaji + bidii, hicho ndicho kizazi cha leo ndio maana Ronaldo ni mfano kwa vijana wengi wa kileo ambao ni Matozi, wanatamani kuwa kama yeye kila idara kuanzia Utozi hadi uwanjani, hayo ndio maisha ya kileo.

Messi anachojua ni kucheza mpira tu , anachojali ni kuhusu kipaji pekee ,hajali ubishoo nje ya uwanja ,hana skendo ambazo wanazipenda mabishoo ,yeye ni ball tu, ndio maana ukiwauliza hata vijana wengi wa Amerika kusini kwasasa wanamkubali Cristiano.

Messi anataka awape kipaji tu ,lakini vizazi vyaleo vinahitaji vitu vitatu UBISHOO + KIPAJI + BIDII kama Cristiano Ronaldo, Alejandro hana dhambi kama wanavyoamini, Garnacho anaenda na upepo unavyoitaji.

Tayari kijana ametemwa timu ya Taifa na kocha akiulizwa anajibu kijana hana takwimu za kuingia Argentina, kwa umri wake hahitaji takwimu kuitwa timu ya Taifa maana anatafuta uzoefu tu ni sababu kaleta Kocha lakini matukio yake ya kumuiga Ronaldo ndio yanasababisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live