Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gari la Wananchi limewaka huko Sauzi

Abuya Maxi Gari la Wananchi limewaka huko Sauzi

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Young Africans SC juzi ilipokea kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya Augsburg ya Ujerumani kwenye michuano ya Mpumalanga Premier International Cup 2024 yanayofanyika Afrika Kusini.

Augsburg walitangulia kupata magoli 2 na baadae Young Africans SC ilipata goli moja la kufutia machozi kupitia kwa mshambuliaji Jean Baleke dakika ya 81.

Mchezo huo ambao uliwapa fursa Young Africans SC kujaribu wachezaji wao wapya kuelekea msimu ujao na mashabiki wakishuhudia maingizo mapya kwenye kikosi hicho.

Asilimia 95 wachezaji wapya wa Yanga wamecheza vizuri, na ndio waliobadilisha RHYTHM ya timu kipindi cha pili.

Clatous Chama; Ni Chama pekee ndiye bado kidogo hajaelewana na wenzie pale juu, akijua jinsi ya kucheza nao Yanga inaenda kuwa tishio zaidi.

Aziz Andambwile; Typically holding Midfielder

Andambwile ni kiungo mkabaji halisi ambaye ameonesha ubora timu inapokuwa na mpira na isipokuwa na mpira. Alienda ku-DICTATE pale katikati na kuipa timu balance inaposhambulia na inaposhambuliwa.. Japo kacheza kipindi cha pili pekee.

Height + Stronger + passer, Aucho kapata msaizi sahihi.

Chadrack Boka; Modern Wing-back Kacheza dakika chache akaumia, ,kafanya safari (3) tu wajerumani Ulimi ndala ..Ule upande aliokuwa anacheza na Max utazitesa sana timu nyingi.

Ana height nzuri, kasi na nguvu za miguu .. Nilikuwa nashangaa akiugusa mpira kidogo unatembea kwa kasi na ujazo aliokadilia na unamfikia mlenga.

Jean Baleke; Watu walikuwa wanahoji kwa nini hatambulishwi ?! Baleke kajitangaxa mwenyewe pale Mpumalanga, Yuko sharp, Nguvu, ni presser mzuri haina haja ya kumzungumzia sana alishajieleza.

Duke Abuya; Pangeni vikosi vyenu vyote ila MAXI hawezi kukaa nje. Kaongezeka MAXI mwingine anaitwa Duke Abuya.

Huyu hakusajiliwa kwa mbwembwe lakini niliwaambia atawashangaza.. Gamondi akijiroga ampe game time ya kutosha anachukua namba ya kidumu kule pembeni.

◉ Yuko fiti muda wote ◉ Work-rate yakutosha muda wote ◉ Ana dribble vizuri kuelekea mbele kwenye final third ya mpinzani.

Gari limewakia kwenye gia, sasa ni jukumu kwa timu za Tanzania kupunguza magoli.

Young Africans SC wataendelea kusalia Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo mwingine wa michuano ya Toyota Cup 2024 dhidi ya Kaizer Chiefs.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live