Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya England Gareth Southgate, amekiri Raheem Sterling “hana furaha kabisa” baada ya kuachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo.
Sterling mwenye umri wa miaka 28 ni mmoja wa wachezaji wenye uzoefu mkubwa na timu ya taifa lakini hajaongeza mchezo wowote kwa timu hiyo tangu ile 82 alipocheza kwa mara ya mwisho Desemba, mwaka jana wakati wakitolewa katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa.
Sterling alikosa mechi ya England iliyochezwa mwezi Machi, mwaka huu kutokana na jeraha na tatizo la misuli ya paja lilipelekea kile ambacho kambi yake ilieleza kama “uamuzi wa pande zote mbili” wa kuzingatia kuuponya mwili wake baada ya msimu wa kwanza kule Chelsea.
Lakini Mshambuliaji huyo hakupokea wito aliotarajia baada ya kuanza vyema msimu huu, huku Southgate akimwacha kwa mechi ya kufuzu kwa Euro 2024 dhidi ya Ukraine itakayochezwa wiki ijayo na ile ya kirafiki kule Scotland.
Ili kumrejesha Raheem ni lazima tumwache mtu mwingine nje na sikufikiria kuna mtu yoyote katika kundi hili la wachezaji washambuliaji anastahili kuachwa.
“Ni vizuri sana kumwona akianza msimu vizuri sana. Anaonekana katika hali nzuri, anaonekana ana njaa. “Ni wazi ni mchezaji muhimu kwetu na amekuwa mchezaji muhimu.
“Lakini katika maeneo hayo ya ushambuliaji tuko nyuma tu ya zile tisa ushindani mkubwa wa nafasi. “Nadhani wachezaji hao wote wameanza msimu vizuri na hakika kundi ambalo tuko pamoja nasi limefanya vyema kwa ajili yetu katika michezo ya hivi majuzi.”
“Hakupatikana kwa mechi mbili zilizopita na bila shaka hiyo imewapa watu wengine nafasi ya kucheza vizuri na kujimarisha kwenye kundi.
“Ni uteuzi mgumu na Raheem hajafurahishwa haswa kuhusu hilo, lakini ninaelewa hilo kwa sababu ni mchezaji muhimu kwetu. “Nina hakika atakuwa na msimu mzuri na Chelsea, hakuna shaka juu ya hilo.”
Southgate aliamua kumpigia simu Sterling kuhusu uamuzi wake kwani alijua kwamba amekuwa “mchezaji mkubwa sana kwetu” na alitaka kutambua jinsi amekuwa akicheza vizuri.
“Raheenm huwa anaheshimu sana jinsi anavyojibu na kushughulikia mambo,” aliongeza Southgate. “Siku zote atasema tazama, naheshimu uamuzi wako’ lakini bila shaka anataka kurejea kundini. Na sitarajii hivyo kwa njia nyingine yoyote.”
Fowadi huyo ameanza mechi tatu za kwanza za Ligi Kuu England akiwa na Chelsea msimu huu, akifunga mara mbili na kutoa asisti katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Luton ljumaa iliyopita.