Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gareth Bale Atarejea Tena Spurs?

Tetesi Za Soka Bale Gareth Bale

Thu, 9 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tottenham Hotspur inaripotiwa kutafakari kuungana tena na Gareth Bale kwenye dirisha la usajili la Januari.

Licha ya panda shuka wakati wa mkopo wa msimu mzima huko London Kaskazini msimu wa 2020-21, Bale alichangia mabao 15 na asisti nne. Tottenham pia walitajwa kuwa hawana mpango tena na Bale.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales amerejea katika klabu mama ya Real Madrid, ambako amebakiza miezi saba katika mkataba wake na mpaka sasa hakuna taarifa au mipango ya wazi ya kuongezewa mkataba.

Kwa mujibu wa mwanahabari Ekrem Konur, kipindi cha tatu ndani ya Spurs kinaweza kuwa chaguo pekee ikiwa Antonio Conte ataidhinisha mpango huo.

Huku wakiwa wanakosa msaada wa Harry Kane, ukiacha na chipukizi Dane Scarlett, timu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza inaweza kuingia sokoni kumnunua mchezaji mpya kwenye safu ya ushambuliaji mwezi Januari.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 hajaichezea Real tangu Agosti kutokana na changamoto ya jeraha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live