Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondia afunguka alichowaambia wachezaji wake mapumziko

Gamondi Miguel Tizi Gamondia afunguka alichowaambia wachezaji wake mapumziko

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa, amefunguka alichowaambia wachezaji wake wakati wa mapumziko kwenye mchezo wa jana dhidi ya Mashujaa FC baada ya wachezaji hao kuumia wakati mchezo ukiendelea.

Gamondi amesema hayo wakati akizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa mchezo huo huku Yanga ikionekana kusua sua kupata matokeo katika michezo yake mitatu iliyocheza ikitoa sare moja na kushinda miwili, ikifunga mabao matatu na kufungwa bao 1.

"Mpira ni mchezo mzuri sana, wakati mwingine una matokeo ambayo hayatabiriki. Kipindi cha kwanza tulipata penati lakini refa aliuma kipenga, ilitulazimu tucheze wa jitihada zote kutafuta bao.

"Tumemiliki mpira vizuri tangu kipindi cha kwanza na kufanikiwa kupata bao, niliwaambia wachezaji wangu tunatakiwa tuwe makini kwa sababu bao moja si chochote, lakini kosa moja lilituadhibu wakarudisha, ikawa ngumu kwetu kusawadhisha.

"Lakini kutokana na uwezo wa wachezaji, ari yao ya kujitoa kupambana walifanya kila kitu wanachotakiwa kufanya na mwisho wa siku tukaondoka na alama tatu," amesema Kocha Gamondi.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC, uliopigwa katika Dimba la Azam Complex, Chamazi, Yanga iliibuka na ushindi wa bao 2-1, dakika za lala salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live