Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi na mtihani wa ‘combination’ Yanga

Gamondi Kambi Gamondi na mtihani wa ‘combination’ Yanga

Fri, 8 Sep 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kama kuna eneo ambalo Kocha Miguel Gamondi linaweza kumuumiza kichwa basi ni eneo la viungo wa ushambuliaji.

Tofauti na misimu kadhaa iliyopita Yanga safari hii ina machaguzi ya kutosha kwenye eneo la kiungo cha ushambuliaji.

Machaguzi haya zaidi yamechagizwa na ujio wa viungo Max Nzegeli na Pacome Zouzoua. Wanafanya Yanga wala isiwaze kuondoka kwa Fei Toto na zaidi imepeleka shida ambayo kila kocha angeweza kuifurahia.

Nasema ni shida ambayo kila kocha angeweza kuifurahia kwa sababu ni bora uwe na machaguzi mengi mazuri kuliko kukosa kabisa au kuwa nayo machache.

Hapa kazi ipo, kocha anakuna kichwa namna ya kuwatumia nyota wake ambao viwango vyao vimewaka na wanawapa kicheko mashabiki huko mtaani wakitamba.

Yanga msimu huu inaonekana kuwatishia amani wapinzani wao, kulingana na dozi iliyotoa katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC na JKT Tanzania zilizochapwa mabao 5-0 kila moja.

Acha na hiyo ishu, tuwazungumzie hawa jamaa walioanza kujitengenezea ufalme wao ndani ya Yanga, hao si wengine ni Max, Stephane Aziz KI, Pacome, Kenneth Musonda na Hafiz Konkoni ambao wanaunda utatu hatari.Mwanaspoti linakuletea baadhi ya muunganiko kwenye wa ushambuliaji ambao hadi sasa Yanga ikiwa imecheza mechi sita mbili Ligi ya Mabingwa Afrika mbili Ligi Kuu Bara na mbili Ngao ya Jamii.

Maxi, Aziz Ki, Pacome

Ni pacha ambayo haijawahi kuanza mchezo pamoja lakini kutokana na mabadiliko ya kocha wakajikuta wanacheza pamoja na kuongeza furaha kwa mashabiki.

Wachezaji hao walikutana kwenye mchezo dhidi ya Asas FC ambao waliingia kuchukua nafasi ya Moloko ambaye alitolewa.

Ni mchezo ambao Yanga ilishinda mabao 5-1 na Pacome aliingia nyavuni mara moja kati ya mabao hayo.

Maxi,

Musonda, Aziz Ki

Utatu mwingine ambao umekuwa chanya kwa Max ni pale anapocheza eneo la mbele sambamba na Aziz KI na Musonda.

Mfano ni kwenye mechi ya ligi dhidi ya JKT Tanzania Yanga ikishinda 5-0, watatu hao walianza kwa pamoja kikosini wakicheza nyuma ya mshambuliaji.

Maxi alikuwa akicheza kama winga sambamba na Musonda huku Aziz akisimama nyuma ya mshambuliaji wa kati, Hafiz Konkoni lakini hata hivyo, walikuwa wakicheza kwa maelewano makubwa na kubadilishana nafasi jambo lililowachanganya mabeki wa JKT na kushindwa kubaini wamkabe nani katika eneo gani.

Kwenye mchezo huu utatu huo ulicheza pamoja kwa Maxi kutumika dakika 90, Musonda 78 na Azizi Ki alicheza dakika 83 na wote alihusika kwenye ushindi wa mabao 5-0.

Aziz Ki, Musonda, Yao wote walitupia bao mojamoja Maxi akiingia kambani mara mbili, ukiachana na ubora waliouonyesha dhidi ya JKT Tanzania watatu hao pia walicheza pamoja dhidi ya Asas FC mechi ya Ligi ya Mabingwa huku Aziz Ki akifunga bao moja na Musonda moja.

Maxi Musonda, Moloko

Utatu huo haukuzaa bao lolote lakini wachezaji waliweza kumudu mchezo kuanzia dakika 45 za kipindi cha kwanza hadi mwisho wa mchezo.

Mchezo huo ulikuwa ni wa fainali Ngao ya Jamii iliyochezwa Jijini Tanga dhidi ya Simba kufanikiwa kutwaa taji ambalo lilikuwa linashiokiriwa na Yanga kwa mkisimu miwili.

Moloko alitumika kwenye mchezo huu kutokana na utimamu wake huku Pacome ambaye sasa amekuwa akicheza kikosi cha kwanza mara kwa mara aliingia dakika za mwishoni.

Maxi, Farid, Musonda

Utatu huo ulicheza pamoja na kuisaidia timu kupata matokeo yaliyowavusha hadi hatua ya fainali baada ya kushinda mabao 2-0.

Kwenye mchezo huo dhidi ya Azam FC bao la kwanza lilifungwa na Aziz KI na la pili lilifungwa na Clement Mzize ambao wote waliingia wakitokea benchi.

Maxi, Moloko, Azizi KI

Mchezo wa mwisho kufuzu hatua ya kwanza Ligi ya Mabingwa dhidi ya Asas FC, Gamondi aliwatumia mawinga wawili Maxi na Moloko huku Aziz KI akikaa nyuma ya mpira, utatu huo iliongeza idadi ya mabao kutoka 2-0 hadi 5-1.

Maxi ndiye aliyefungua kwa kuifungia Yanga bao la kwanza bao la pili lilifungwa na mshambuliaji Konkoni yalidumu hadi mapumziko huku mabao ya Mzize na Pacome wakifungwa kipindi cha pili.

Maxi alirudi tena kambani kuikamilishia Yanga idadi ya mabao matano waliyoyapata dhidi ya Asas FC ambao walifunga bao moja la kufutia machozi.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: