Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi na mitihani mitatu Yanga

Gamondi Yanga Ms Gamondi na mitihani mitatu Yanga

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi anakabiliwa na mitihani mitatu mbele yake leo, Jumapili saa 2:30 usiku wakati akiwaongoza Wananchi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mitihani hiyo ni kuhakikisha analinda mbinu zake kutokana na Mamelodi Sundowns F.C. kuutumia mchezo huo kama kilele cha kuisoma Yanga kabla ya kukabiliana nao wikiendi ijayo, Machi 30 kwenye robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mchezo uliopita wa ligi, Gamondi aliwapiga chenga watu wa Mamelodi ambao walikuwa Azam Complex, Chamazi kwa ajili ya kuwafuatilia wakati wakikabiliana na Geita Gold, kocha huyo alipangua kikosi chake cha kwanza kwa lengo la kutunza nishati kwa ajili ya mchezo wa leo.

Bila shaka leo, Jumapili kocha huyo anaweza kutumia wachezaji wake muhimu akiwemo Mudathir Yahya, Pacome Zouzoua, Kouassi Attohoula Yao na Ibrahim Hamad 'Bacca' ambao wote hawakuanza wakati wakiwavaa wachimba madini wa Geita, mtihani utakuwa ni kwa namna gani hatonasa kwenye kile ambacho Wasauzi hao wanakihitaji.

Mtihani wa pili ni kuhakikisha wachezaji wake wanamaliza salama mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani wa aina yake, bila ya kupata majeraha ambayo yanaweza kuvuruga mipango yake.

Wakati akipiga hesabu hizo lakini pia anatakiwa kuhakikisha anakusanya pointi kwenye mchezo huo ili kuendelea kujikita kwenye kilele cha msimamo wa ligi ambayo anaongoza akiwa na pointi 52 kama watadondosha pointi ina maana watatoa mwanya kwa Simba (45) na Azam (44) kuwasogelea.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: