Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi na Nabi leo patachimbika

Kaizer V Yanga Gamondi na Nabi leo patachimbika

Sun, 28 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo ni moja ya siku ambayo mashabiki na wapenda soka wanatamani muda ukimbie kwa hamu ya kutamani kuona mtanange baina ya Kaizer Chiefs dhidi ya Yanga.

Miamba hiyo itashuka dimbani saa 10:00 jioni katika mechi ya Toyota Cup itakayopigwa nchini Afrika Kusini.

Kaizer kwa sasa inanolewa na aliyekuwa wa Yanga, Nasreddine Nabi ambaye aliacha alama kubwa Jangwani baada ya kuwafikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga kwa sasa inanolewa na Kocha Miguel Gamondi ambaye amejitengenezea umwamba wake baada ya kuwafikisha robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika na kuchukua mataji mawili ya LigI Kuu Bara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live