Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi kwa nini Mzize?

Mzize Wa Annaba Na Kigali Na Fursa Zake Tatu Mkononi Gamondi kwa nini Mzize?

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moja kati ya karata ya dhahabu ambayo Mwalimu Miguel Gamondi wa Yanga aliisikuma dhidi ya Azam Fc kwa umakini mkubwa bila kuongozwa na presha yoyote ile basi alikuwa ni Clement Mzize.

Kipindi Azam Fc inaongoza bao 2-1 dhidi ya Yanga kuna Shabiki mmoja wa Yanga aliniambia "Inabidi Clement Mzize atoke kwa maana hana faida".

Ni hali ya kawaida hiyo kwa kila shabiki na wala sikumshangaa hasa kwa wale ambao hawalipi Jukwaa ile kitu roho inapenda lakini wanampa Mwalimu ile kitu roho inapenda .

Malickou pamoja na Daniel Amoah kuna mtego waliingia wote kwa Clement Mzize, waliona kutokana na umri wake mdogo kama wakimfanyia high pressing basi atapoteza mipira kwa wingi na itakuwa udhaifu mkubwa sana kwa Yanga.

Ni kweli kipindi cha mchezo Malickou na Amoah walijitahidi sana kufika kila sehemu ambayo Mzize alipokea mpira lakini Mzize ni full package, Mzize hakuwa na presha dhidi ya Mabeki hawa wa Azam.

Alikuwa anatulia kwenye presha anawasubiri Amoah na mwenzake waje kufanya pressing juu yake huku wakiwaacha akina Stephanie wakiwa huru sana, wengi hawakuona umuhimu wake.

Lakini Gamondi nahisi alijua uwepo wa Clement unachangia kutengeneza nafasi kwa wachezaji ambao wapo pembeni ya uwanja maana alikuwa anajua kuilinda mali pindi akifanyiwa pressing na mabeki wa Azam FC.

Mzize ni kijana anayechipukia kwenye ushambuliaji, ni full package, hata asipofunga kuna kitu anakitoa kimbinu na kuifanya timu yake ipate matokeo.

Ndiyo maana Gamonsi anamchagua kuwa mshambuliaji wake namba moja licha ya kuwa na Kennedy Musonda na Hafiz Konkoni, kuna vitu akiviongeza nina imani atafika mbali sana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: