Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi kuisuka upya safu ya ulinzi Yanga

Nondo Job Bacca Gamondi kuisuka upya safu ya ulinzi Yanga

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa watafanyia kazi makosa katika mechi za kimataifa upande wa ulinzi ili kutoruhusu mabao mengi ya kufungwa.

Ipo wazi kuwa katika mechi mbili ilizoshuka uwanjani hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, ukuta wa Yanga uliokota mabao manne, ugenini dhidi ya CR Beloizdad ilitunguliwa mabao matatu na Uwanja wa Mkapa dhidi ya Al Ahly ni bao moja.

Gamondi amesema kuwa makosa waliyofanya kwenye mechi za kimataifa ni sehemu ya mchezo jambo ambalo linafanyiwa kazi katika uwanja wa mazoezi.

“Utaona kwamba mabao ambayo tulifungwa ilitokana na namna ya kuzuia makosa ambayo tulifanya. Hapo ni muhimu kwetu kuangalia namna ya kurejea katika ubora na sehemu ya mazoezi tunafanyia kazi hayo.

Kikubwa ni kuona kwamba hatufanya makosa mengi kwenye eneo letu la hatari kwani wapinzani nao wanatafuta matokeo, hivyo hilo tunalifanyia kazi kwa ajili ya kuwa imara kwa mechi zijazo.”

Safu ya ulinzi ya Yanga inayotarajiwa kuvaana na Medeama ya Ghana Desemba 8 inaongozwa na Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Bacca.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: