Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi kiboko, aweka rekodi ya mabao 104 Yanga

Aziz Maxi Mazize Gamondi noma, aweka rekodi ya mabao 104 Yanga

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Young Africans SC wamebakiwa na mechi mbili pekee kuhitimisha msimu wa 2023-2024 huku wakiwa tayari wana taji moja la Ligi Kuu ya NBC ambapo leo Jumanne wanacheza mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya Tanzania Prisons.

Baada ya hapo, wanaufunga rasmi msimu Jumapili kwa kucheza fainali ya CRDB Federation Cup dhidi ya Azam ambapo wanakwenda kwa ajili ya kutetea taji lao lingine.

Wakiwa wanazielekea mechi hizo mbili zilizobaki, Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi amefanikiwa kuweka rekodi ya aina yake ndani ya kikosi.

Rekodi hiyo ni ya timu kufunga magoli mengi zaidi katika michuano yote ambayo wameshiriki msimu huu wa 2023-2024.

Mpaka sasa, Young Africans imefunga jumla ya magoli 104 ambayo ni mengi zaidi ikiwa ni rekodi ya jeshi la Gamondi ambaye ana msimu mmoja pekee ndani ya timu tangu ajiunge nayo Juni 2023.

Mchanganuo wa magoli hayo upo hivi; Kombe la FA (16), Ligi ya Mabingwa Afrika (19), Ligi Kuu ya NBC (67) na Ngao ya Jamii (2).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live