Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi hesabu zake kwa Azam FC fainali ya Kombe la Shirikisho

Yanga Pacome Gamondi Zdc Gamondi hesabu zake kwa Azam FC fainali ya Kombe la Shirikisho

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati leo Jumanne wakitarajia kucheza mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tanzania Prisons, Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi amesema ataingia kwa tahadhari kwani bado kuna mchezo mwingine muhimu mbele yetu.

Mchezo huo muhimu zaidi ujao baada ya leo ni wa fainali ya CRDB Bank Federatin Cup tutakaocheza dhidi ya Azam, Jumapili ya Juni 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Young Africans itaingia kwenye mchezo huo ikiwa bingwa mtetezi huku malengo yakiwa ni kutetea ubingwa huo baada ya kufanikiwa kufanya vizuri ndani ya ligi.

“Usisahau kwamba ni mwisho wa msimu, kuna wachezaji waliocheza muda mwingi na wengine hawakupata nafasi kubwa na wanastahili kuipata katika mechi rasmi.

“Hii inanipa nguvu kuona wachezaji wanataka kuonesha kitu cha ziada, lakini tunapaswa kutunza nguvu kwani Jumapili tuna fainali ambayo ni muhimu sana.

“Tunatakiwa kulinda hali ya uchovu, kadi za njano, ari ya kupambana na mengine mengi jambo ambalo tunaweza kufanya mabadiliko ya kikosi lakini siyo makubwa sana,” alisema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live