Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi hana presha na Simba

Gamondi Ms Gamondi hana presha na Simba

Sat, 12 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa Klabu ya soka ya Young Africans, Miguel Gamondi amesema kuwa yeye na benchi lake la ufundi hawawezi kuwapa presha wachezaji wao kuelekea mchezo wa fainali ya ngao ya jamii dhidi ya Simba Sc.

Gamondi amesema hayo baada ya kuulizwa na wanahabari kuhusu maandalizi ya kikosi chake dhidi ya mpinzani wake huyo ambapo mchezo huo utapigwa kesho Jumapili katika Dimba la CCM Mkwakwani Tanga.

"Siyo mimi tu, hata bench langu la ufundi na viongozi hatuwezi kuwapa pressure wachezaji wetu kwa kuizungumzia Simba kwasababu sio timu pekee tutakayoshindana nayo ligi kuu, napenda nizungumzie timu 15 tutakazoshindana nazo katika michezo 30 ya ligi" amesema Gamondi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: