Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi awataja wanaomrahisishia kazi ya ushindi Yanga

Gamondi Kambini Yanga Gamondi awataja wanaomrahisishia kazi ya ushindi Yanga

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kutangazwa kuwa kocha bora wa Februari akimpiku kocha wa Simba, Abdelhak Benchikha, kocha wa Yanga Miguel Gamondi amesema ni matunda ya ushirikiano mzuri baina yake na wasaidizi wake.

Pia amewataja wachezaji wake kuelewa zaidi mfumo wake na ana kikosi kilicho na vipaji vingi, kitu ambacho kimechangia mafanikio anayoyapata sasa ndani ya timu hiyo.

"Lakini pia wasaidizi wangu wanafanya kazi na ushirikiano mkubwa huku wakichangia kwa kiasi kikubwa timu kuwa na mabadiliko siku hadi siku," anasema.

"Kuna kocha wa viungo, kocha wa makipa, meneja wa timu waratibu wa timu na viongozi wote nimekuwa nikifanya nao kazi kwa ukaribu wote tukiwa na lengo moja kuhakikisha tunafikia malengo."

Gamondi anasema tuzo huyo pia anaikabidhi kwa mashabiki wa Yanga ambao wamekuwa na hiyo timu nyakazi zote kuipa nguvu inapopambana kwenye hali nzuri na mbaya.

Kocha huyo ameshinda tuzo hiyo baada ya kuiongoza Yanga kwenye michezo mitano ikishinda minne na suluhu moja na kupanda kutoka nafasi ya pili hadi ya kwanza. Aliiongoza dhidi ya Kagera Sugar (0-0), akashinda dhidi ya Dodoma Jiji bao 1-0, Mashujaa 2-1, Tanzania Prisons 1-2 na KMC 0-3.

Hiyo ni tuzo ya pili kwa kocha huyo baada ya kutwaa ya mwezi Agosti ambayo alikabidhiwa muda mfupi kabla ya mchezo dhidi ya Namungo ugenini wakishinda mabao 3-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: