Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi awapa masharti mazito Yanga, wachague yeye au Okrah

Gamondi X Okrah  . Gamondi awapa masharti mazito Yanga, wachague yeye au Okrah

Tue, 18 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Inasemekana kuwa Augustine Okrah kutoka Ghana hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga cha msimu ujao.

Mazungumzo kati ya pande zote mbili yamefanyika na mchezaji huyo amevunjiwa Mkataba.

Viongozi wa klabu ya Yanga wanataka Okrah abaki lakini kocha anasema Okrah hayupo kwenye mipango yake.

Inasemekana kuwa Gamondi ameenda mbali na kuitaka Yanga ichague kati yake na Okrah, nani abaki.

Kocha huyo pia amesema kama Yanga watamruhusu Okrah abaki ndani ya klabu hiyo basi atakwenda kufanya mazoezi na U-20.

Ikumbukwe kuwa Yanga bado ina deni la Okrah, mishahara na bonasi za ushindi lakini waliahidi kuwa watalipa.

Iwapo kama hawatalipa kwa muda uliopangwa, Okrah na wanasheria wake wataipeleka Yanga FIFA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: